Header

Arsenal hoi mbele ya Watford,Ndoto za Ubingwa wa Ligi kuu England zayeyuka

Nadiliki kusema ndoto za Klabu ya Arsenal kutwaa ubingwa wa England yanaanza kufifia baada ya kuchapwa na Watford 2-1 kwenye mchezo wao wa 23 wa Ligi kuu ya England.

Odion Ighalo akishangilia goli lake la kwanza kwenye mchezo huo Watford wakiibuka na ushindi wa Goli 2-1 dhidi ya Arsenal.

Odion Ighalo akishangilia goli lake la kwanza kwenye mchezo huo Watford wakiibuka na ushindi wa Goli 2-1 dhidi ya Arsenal.

Mlinzi wa zamani wa Tottenham Younes Kaboul alianza kuiandikia Watford goli la kwanza dakika ya 10 baada ya kuachia shuti kali lililomgonga Aaron Ramsey na kutinga nyavuni.

Dakika mbili na sekunde 57 baadaye Troy Deeney akaiandikia goli la pili Wtaford baada ya mpira uliopigwa na Etienne Capoue kupanguliwa na mlinda mlango Petr Cech na kisha kumkuta Troy aliyeandika bao safi.

Kipindi cha pili Arsenal walianza kwa kasi na kujipatia goli la kufutia machozi kutoka kwa Alex Iwobi baada ya kupanda pande safi lililochongwa na Alexis Sanchez.

Kwa mara ya mwisho Arsenal kushinda kikombe cha ligi kuu England ilikuwa msimu wa mwaka 2003-04 na kwa sasa wapo nyuma kwa alama tisa dhidi ya vinara Chelsea ambao wametoka suluhu ya 1-1 dhidi ya Liverpool.

Comments

comments

You may also like ...