Header

Mrembo Avril atatumia njia hii kupata mtoto kama atakosa Mwanaume mwenye sifa anazozihitaji

Msanii mrembo kutoka Kenya Avril wiki iliyopita alishangaza wengi baada ya kutamka mbele ya kadamnasi kuwa yupo Tayari kutumia njia mbadala kupata mtoto lakini sio kubebeshwa mimba na mwanaume asiyempenda.

Image result for avril kenya

Mrembo huyo alifunguka yote hayo alivyokuwa akihojiwa na Kituo cha Radio cha Kiss FM na kusema sasa ameanza kuwazia kupata mtoto kwa kutumia mbinu ya Kisasa ya kupandikiza Mbegu za Kiume endapo hatampata mwanamume mwenye sifa zake.

Kwa sasa nipo singo na kama sitafanikiwa kumpata mwanamume mzuri wa kunipa ujauzito basi nitatembelea kituo cha IVF kusaka mbegu” Alisema Avril.

Siku chache zilizopita Avril ambaye kwa sasahivi yupo single aliposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonesha akiwa mjamzito lakini baadae akaibuka na kusema alikuwa anatania tu!! na kuwa ujauzito huo ulikuwa wa kubandika.

Avril ameendelea kugonga vichwa vya habari nchini Kenya hususani kwenye Majarida na Magazeti ya Udaku Mengi yakihoji mahusiano yake tangia alipotemana na mchumba wake Muga.Hata hivyo cha wazi ni kuwa Avril tangu aachane na Muga mawazo yake hayajaonekana kutulia hasa kuhusiana na hali yake ya upweke.

Comments

comments

You may also like ...