Header

Haji Manara apewa ruksa ya kutafuta Refa wa kuchezesha mchezo wa Simba na Yanga

Kama unakumbukumbu nzuri ni kwamba  Msemaji wa Simba Haji Manara amekuwa akisisitiza mechi dhidi ya watani wao Yanga ichezeshwe na mwamuzi kutoka nje ya nchi.
Jerry Muro na Haji Manara

Jerry Muro na Haji Manara

Sasa Chama cha Waamuzi Tanzania (Frat) kimempa Manara kazi ya kutafuta Refa atakayeweza kuchezesha mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga kwa kufuata weledi ya sheria 17 za soka.
Kwa kuwa watani hao wanatarajia kukutana Februari 25, mwaka huu, maana yake Manara ananafasi kubwa ya kumpata mwamuzi huyo.
Simba na Yanga, zinatarajia kukutana katika Ligi Kuu Bara ambapo awali ilipangwa wacheze Februari 18 lakini mchezo huo umesogezwa mbele kutokana na majukumu ya kimataifa ya Yanga.
Mwenyekiti wa Frat, Mwalimu Nassor, amesema bado hawajapanga ratiba ya mwamuzi wa mechi ya watani.
Wakati mwingine hatupendi malalamiko, maana kila timu inayofungwa au kuzidiwa ndiyo hulalamika. Basi yeye atafute huyo mwamuzi ili tupunguze lawama,” Amesema Mwalimu Nassor.

Comments

comments

You may also like ...