Header

Ngoma zangu zinabaniwa redioni – Cassper Nyovest

Aliumaliza mwaka 2016 kwa kishindo baada ya kuujaza uwanja wa mpira wa Orlando, lakini haina maana kuwa hakutani na vikwazo. Rapper Cassper Nyovest amelalamika kuwa vituo vya redio vya nchi kwao, SA, vinambania.

Amedai kuwa vituo vya redio vimeikanyagia album yake, Refiloe lakini anaamini kuwa hawampunguzii kitu. Rapper huyo amejigamba kuwa ameanda bomu jingine ambalo hawawezi kulikwepa.

“They slept on my whole album bro. Monate so, 428 to La , Malome, Find My Way, Cooking in the kitchen and Fever should have been BIG SONGS,” alimjibu shabiki kwenye Twitter.

“It doesn’t hurt me anymore that people slept on Refiloe as an album cause I got a better project on the way. My best work yet. Undeniable,” aliongeza.

Comments

comments

You may also like ...