Header

Bondia Mohammed Matumla bado yupo ICU baada ya Kipigo cha KO juzi

Bondia Mohamed Matumla bado hali yale kifya ni Tete baada ya Kupigwa KO na Mfaume Mfaume kunako raundi ya ya Saba kwenye pambano ambalo sio la Ubingwa.

Mohammed Matumla ambaye ni mtoto wa mchezaji masumbwi wa zamani Rashid Matumla bado amelazwa hospitali ya Temeke ambapo amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi ICU .

Akiongea na DizzimOnline Baba mzazi Rashid Matumla amesema kwasasa hali ya mgonjwa inaendelea vizuri ingawaje bado yupo ICU ila hali ikiendelea vizuri zaidi huenda akatoka baada ya siku mbili.

Kidogo hali ya mgonjwa kuanzia jana na leo inaridhisha ingawaje bado yupo ICU na ningependa pia kuwaomba watanzania hususani wadau wa Michezo watusaidie kwa chochote walichonacho kwani gharama zimeongezeka na hali ya uchumi sio nzuri“Amesema Rashid Matumla.

Comments

comments

You may also like ...