Header

Nikki Mbishi ataja Marapa watano anaowakubali Bongo

Rapa kutoka TamadunMuzik Nikki Mbishi ni moja kati ya Marapa wanaofanya vizuri sana hapa nchini,na endapo utamuuliza ni wasanii gani wa Hip Hop anaowakubali basi kwenye hiyo orodha hutakosa kuona jina la Hashim Dogo.

Related image

Nikki Mbishi anaefanya vizuri kwasasa na wimbo wake wa ‘I’m sorry JK’ ametaja Orodha yake ya Wasanii watano ambao ni Mbunge wa Jimbo la Mikumi Professor Jay,Hashim Dogo,Fid Q,One The Incredible na Stereo.

Akitaja majina hayo kwenye Kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio amesema watu wengi hawamfahamu Hashim Dogo ila kwake yeye  anamuona ni MC mkubwa sana wa Hip Hop.

Comments

comments

You may also like ...