Header

Young Killer: Simuogopi na sijawahi kumchekea Young Dee

Rapper Young Killer amekanusha uvumi kuwa alikuwa akimchekea Young Dee baada ya wao kukutana kwenye studio ya Mona Gangster na kusema kuwa hamuogopi rapper huyo.

Young Killer akijibu swali la Dizzim Online, Je ni kweli alimuogopa Young Dee baada ya wao kukutana, amesema, “mimi nimezaliwa kufurahi kwahiyo nilipomuona nilicheka kutokana na story nilizopiga na watu wengine na sio nilimchekea yeye.”

Uhusiano kati ya wawili hao umeharibika tangu Young Killer amchane Dee kwenye wimbo wake Sinaga Swagga.

Comments

comments

You may also like ...