Header

Walichofanya Fid Q na Joh Makini liwe somo kwa Ali Kiba na Diamond Platnumz

Kuna msemo mmoja wa kimombo unaosema ‘ Two bulls can not rule in one kraal ‘ Ukiwa na maana ya ‘ Fahari wawili hawakai zizi moja ‘ .Ni jambo linaloweza kuwa na usawa kwa upande mmoja lakini sio kwa Marapa wawili wakongwe Tanzania FID Q na JOH MAKINI,kwani wameufanya msemo huo wa wahenga kinyume na tunavyouamini kwa kitendo cha kusapotiana kazi zao kwenye mitandao ya kijamii na kuwaacha watu midomo wazi mpaka hivi sasa.

Kwa kipindi kirefu Fid Q na Joh Makini wamekuwa wakishindanishwa kuwa nani ni mkali wa miondoko ya Hiphop? wameshindanishwa mara kadhaa kwenye vipindi vya redio,magazeti,majarida na hata katika Tuzo kubwa Kama KTMA na ubishani ukazidi kuwa mkali hasa pale Joh Makini alipombwaga Fid Q na kunyakua Tuzo ya Mwana Hiphop Bora ya KTMA mwaka 2011.

Tumeona mara kadhaa wasanii wawili walio juu na hasa wanaofanya muziki wa aina moja kuingia kwenye mabifu na huanzia kwenye mambo ya kimuziki na baadae hata Hugeuka na kuwa ni ugomvi wa kibinafsi na sio muziki tena na huenda hata kufikia kupoteza uhai aidha kwa mmoja wao au wote mfano kama sakata la 2PAC na BIG NOTOLIOUS.

Je, unajua hasa chanzo cha haya yote ni nini? Hapa chini nitakuelezea moja ya sababu za wasanii wanaotamba kwa wakati mmoja kuingia katika Bifu kwa mashinikizo kutoka kwenye Media na Mashabiki,huku wakongwe hawa wawili wakiwa wameushinda mtihani huo na kuwapa Funzo kwa Wasanii wenye ushindani mkubwa kwa sasa katika muziki wa Bongo fleva nao ni ALI KIBA na DIAMOND PLATNUMZ.

MASHABIKI

Sio mara zote wasanii wakiingia katika bifu basi huwa chanzo ni wao wenyewe mara nyingine huwa ni mashabiki ndo husababisha msanii mmoja kutofautiana na msanii mwingine kimuziki.

Ushindani wa Diamond na Ali kiba umechangiwa hasa na mashabiki kujigawa na kila mmoja kumsapoti msanii wake na hapo ndipo zikaundwa Team za Mashabiki zenye Lengo hasi la kumshusha mmoja wao ili mwingine awe juu.

Hivyo ndivyo ilivyotokea Kwa Fid Q na Joh Makini ambapo mashabiki walichangia kwa kiasi kikubwa sana Kuchochea Bifu ya Joh Makini na Fid Q kwa Lengo la kisingizio cha kuchangamsha gemu ya Hip Hop lakini wapi Wawili hao wameweza kuwarudisha mashabiki kwenye mstari uliosahihi .

MEDIA

Hakuna ubishi nafasi ya Media kwenye Jamii ni kubwa sana sio kwenye kipindi hiki ila toka Enzi kwani hata vita zinazoendelea huko kwenye mataifa ya wenzetu chanzo kikubwa ni Vyombo vy Habari iwe ni kupindisha kauli au kukuza mambo ambayo yataleta athari kwenye jamii.

Tukirejea kwenye Bifu za wasanii kuna  baadhi yao yanaanzia nje nje iwe ni kutofautiana kikazi lakini media huyakumbatia na kuyakuza ,Kama nilivyosema awali Media nyingi yakiwemo Magazeti,Majarida,Radio na Tv ziliwashindanisha kila uchwao Marapa hawa wawili katika vipindi vyao .

Hivyo hivyo hata kwa tofauti iliyopo kati ya Ali Kiba na Diamond Platnumz kufikia hapa ambapo kila mmoja anaganga na yake na kutunishiana misuli kumesababishwa kwa kiasi kikubwa Media kuikuza na kutengeneza mazingira ambayo mpaka sasa Wasanii hao wawili wanayaishi.

Hebu fikiria utajisikiaje kama siku moja ukamuona Diamond au Ali Kiba wakihojiwa kwenye kipindi kimoja cha Radio au Runinga?na vipi kama Leo unaamka asubuhi unamkuta Ali Kiba Kaposti Video Mpya ya Diamond Platnumz na Neyo Marry You kwenye ukurasa wake?au Diamond Kaweka Poster ya US Tour ya Ali Kiba kwenye ukurasa wake wa Instagram?Najua siku hiyo Afrika nzima itakuwa ndiyo habari kubwa kama kipindi kile kule naijeria walivyopatana na Wizkid au pale Marapa wakubwa kutoka South Africa Cassper Nyovest na AKA Walivyopatana na kuweka kando Tofauti zao.

 SOMO LA FID Q NA JOH MAKINI KWA DIAMOND NA ALI KIBA

Waswahili wanasema fimbo ya mbali haiui Nyoka kwani huenda mfano wa Bifu ya Wizkid na Davido au Cassper Nyovest na AKA kumalizika ukawa ni mfano wa Mbali hebu Diamond na Ali kiba jifunzeni kwa kaka zenu Fid Q na Joh Makini ambao wameamua kushinda nguvu za mashabiki na Media ambazo zilitaka kutengeneza pesa kwa lengo la kumshusha mmoja wao.

AKA na Cassper Nyovest baada ya kupatana

Fid q na Joh makini wanaingia katika list ya Wana Hiphop ambao wameweza kushinda majaribu ya kuingia katika bifu kama ambavyo Marapa vijana kutoka South Africa (EMTEE & NASTY C ) ambao kila uchwao hushindanishwa na media zikijaribu kuwaingiza katika Beef.

Fid Q na Joh Makini kama wasingeweza kuwa smart na kukaa chini kutafakari mahusiano yao wangeenselea kuwa kwenye mtafaruku lakini ona sasa Wameweza kushinda mihemko ya mashabiki pamoja na Media na wameamua kuungana na kuupeleka muziki wa Hiphop mbele zaidi na hata kumpelekea Fid q kupost kipande cha wimbo wa Joh makini ‘ WAYA ‘ kuwaomba mashabiki zake waende YOUTUBE kuitazama video ya Joh Makini na kuwatoa Hofu wapenzi wa hiphop wote kuwa wawili hao wako peace.

Natarajia kuona siku moja Timu za kwenye mitandao zikiwa timu za kusapoti Muziki wa Tanzania kwa kila msanii sina maana kusiwe na Timu za msanii binafsi hapana timu ziwepo ila zisiwe na Lengo la kumshusha mtu bali ziwe na malengo chanya ya kukuza muziki wetu iwe kwa kupiga kura au kununua bidhaa zao na sio kushusha muziki wetu kwani nawaza kama tungekuwa na mastaa kumi kama Diamond na Ali kiba basi Tanzania muziki wetu ungekuwa mbali sana.

Sina Imani kuwa tofauti za Wasanii zinaongeza utamu kwenye game mawazo hayo sina ila ninachoamini Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

Makala haya yameandaliwa na kuhaririwa na Godfrey Mgallah kushiriakiana na Fowz Ovyo usitumie kipande chochote cha Maneno kwa matumizi yako Binafsi kutoka kwenye Makala hii.

 

Comments

comments

You may also like ...