Header

Wakali Kwanza ilisharudi kitambo mambo mengine ni Mbwembwe tu – Joslin

Wakali kwanza ni miongoni kati ya makundi yaliyowahi kuvuma na kufanya vizuri kati ya mwaka 2010 kushuka mpaka 2006 na unapoizungumzia Wakali kwanza unazungumzia wasanii watatu wakubwa nao ni Joslin,Q Jay na Makamua.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa mwishoni mwa mwaka jana walitangaza kurudi pamoja baada ya mmoja kati ya member wa kundi hilo kurejea tena (Q Jay) baada ya taarifa za awali kudai kuwa aliachana na muziki wa dunia(aliokoka).

Kupitia kipindi cha XXL mmoja wanaowakilisha kundi hilo Joslin amesema>>’Wakali sio inarudi,Wakali imesharudi kwa sababu project tumeshafanya kazi tumesharekodi kila kitu kinaenda kwenye mstari’

‘Unajua Wakali kwanza ni kundi lenye watu wengi usije kushangaa baada ya hapo watu wanaokuja kuongezeka ongezeka tofauti wasije watu kushangaa labda kuwataja kwa sasa ni miyayusho lakini wapo wengi katikati watakuja kuungana’

‘Watu wategemee watakuja kuwasikia watu tofauti tofauti wanaotokea kundi la Wakali Kwanza kwa sasa watasikia mizigo kutoka kwetu wenyewe ambao ni mimi,Q Jay na Makamua’ – Joslin.

Umeipata hii?Kumbe Y Tony aliwahi kuachwa na Mpenzi wake kisa kikiwa ni Wivu,mtazame hapa.

 

Cheki Wakali Kwanza walipokua pamoja enzi hii ya ‘Natamani’

 

Comments

comments

You may also like ...