Header

Luis Suarez kucheza Fainali ya Kombe la Mfalme?

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Luis Suarez amedai kuwa ana matumaini ya kwamba rufani yake itakayokatwa itaweza kumuokoa asikose mchezo wa fainali ya Kombe la Mfalme baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo wa nusu fainali ya mkondo wa pili dhidi ya Atletico Madrid.

Suarez aliifungia Barcelona bao katika mchezo ambao ulishuhudia wachezaji watatu wakipewa kadi nyekundu katika sare ya bao 1-1 jana iliyofanya Barcelona kufuzu fainali ya nne mfululizo kwa jumla ya mabao 3-2.

Hata hivyo nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay alitolewa nje kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu aliyokaa Barcelona baada ya mwamuzi kudhani alimpiga kiwiko Koke katika dakika za majeruhi.

Suarez amesema kadi hiyo aliyopewa inamfanya ajisikie kucheka kwani inaonekana kama mwamuzi alidhamiria kufanya hivyo. Suarez aliendelea kudai kuwa wanataka kuona kama wanaweza kukata rufani kwasababu hadhani kama alifanya kosa lolote kustahili adhabu hiyo.

Comments

comments

You may also like ...