Header

‘Brand ya African Boy inanilipa zaidi kuliko muziki wangu’ – Jux

Mmoja kati ya waimbaji wazuri wa muziki wa rnb Tanzania,Juma Jux amesema kuwa kama ukiwekwa mzani wa kupima kipi zaidi kinamlipa kwa wakati huu kati ya Muziki na brand yake ya African Boy basi African Boy itakua na uzito zaidi.

Jux kupitia XXL ya Clouds FM amesema>>’ African boy Imenipa pesa ni kitu ambacho kinaniingizia pesa sana,muziki pia unaniingizia hela kwa shows sana,sasa shows zinaweza zisije baada ya mwezi ukafanya shows mbili kuna shows ambayo inakuja pesa nyingi kwa wakati mmoja lakini african boy ni hela ya kila siku’

‘Ukitaka kuhesabia ni hela ipi inaingia vizuri na nyingi unaweza kupiga hesabu then ya African Boy ikawa nyingi kwasababu African Boy inaingiza hela kila siku,siwezi kukaa kwa siku African Boy isiuze haiwezekani ni hela ambayo inaingia kila siku ya Mungu lakini mziki unaweza kukaa week mbili haujafanya shows ikija hela inakuja kwa pamoja nyingi’

‘Hela ya African Boy inasaidia muziki hela ya muziki pia sometimes inasaidia African Boy ni kazi zangu mbili ambazo zinaingiliana kwasababu zinategemeana zote,mimi nisipokuwa mwanamuziki nisipoimba sidhani kama African Boy nitauza na African Boy pia nikisema niache kuuza kuna sometimes kama mwanamuziki hata kama una hela kuna mahitaji yanahitajika zaidi so inabidi utoe huku kwasababu inaibeba brand pia’ – Jux

Uliisikia mipango ya JUX mwaka 2017?kaiweka wazi yote hapa kupitia Dizzimonline.

Comments

comments

You may also like ...