Header

Ben Pol ataja baadhi ya sifa ambazo msanii anaweza kuwa Balozi wa Kampuni

Msanii wa Bongo Fleva Ben Pol ni moja ya Wasanii ambao ni Mabalozi wa WildAid Foundation Tasisi ambayo inalengo la kulinda wanyama pori dhidi ya majangili.

Unaweza ukajiuliza kuna vigezo gani?ambavyo vinazingatiwa ili Msanii aweze kupata shavu la kuwa balozi hususani kwenye Makampuni makubwa ,Ben pol kupitia DizzimOnline amesema kitu kikubwa wanaangalia jinsi msanii unavyoishi kwenye jamii yako kama una skendo au kashfa yoyote ni ngumu sana kukuchukua nyingine ni kujiheshimu wewe mwenyewe na kuonesha kwa dhati uhusiano wako na kile wanachokihitaji.

Mimi nafikiri kujiheshimu,kuishi vizuri,kujitahidi kuepuka skendo na kashfa kwenye jamii yako,hivyo nadhani ni vigezo ambavyo vinaweza kumsaidia msanii kupata Ubalozi kiurahisi,kwani makampuni mengi hayapendi kuchafuliwa kwa kufanya kazi na watu wenye mienendo mibaya kwenye Jamii,mimi nadhani ndiyo vigezo wanavyoangalia zaidi“Amesema Ben Pol

Comments

comments

You may also like ...