Header

Joh Makini aeleza kwanini alienda kufanya media tour Kenya

Sio wasanii wote wa Tanzania wamekuwa na desturi ya kufanya media tour nchi jirani. Lakini mwaka huu Joh Makini aliamua kujifunga kibwebwe na kufanya ziara kubwa kwa vyombo vya habari jijini Nairobi, Kenya ambako alihojiwa kwenye redio na TV zote kubwa.

Akiongea na Dizzim Online, rapper huyo amesema amekuwa akipata simu nyingi za watangazaji wa nchini humo wakitaka kufanya mahojiano naye na ndio maana aliamua kufanya media tour huko.

“So far mabadiliko ni makubwa tu, sasa hivi Napata airtime ya kutosha Nairobi. Nimekuta wimbo kama Don’t Bother ni mkubwa sana Kenya, Perfect Combo ni wimbo mkubwa sana, so naamini itafungua milango mingine ya kukuza na kuendelea kuufikisha muziki wa Joh Makini na hip hop ya Tanzania kimataifa,’ amesema Joh.

Comments

comments

You may also like ...