Header

Lulu Diva-‘Sero ni zaidi ya Shule’

Baada ya kuonja joto la sero kwa siku kadhaa, msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbasi ‘Lulu Diva’ ameibuka na kusema sero ni shule kwani amejifunza mambo mengi.

Image result for lulu diva

Lulu Diva amesema kwenye maisha yake hakuwahi kutegemea kuingizwa sero lakini kwa muda aliokaa, amepata uzoefu mpya ambao hatausahau maishani mwake.

Yaani mle ndani kwangu mimi kila kitu kilikuwa kigeni, mazingira yalivyo, watu waliomo mle kwa kweli si mahali pa kuomba au kutamani kwenda, nimejifunza kwa kweli,” Amesema Lulu Diva.

Lulu Diva pamoja na Wasanii wenzake ambao walihusishwa na tuhuma za madawa ya kulevya, waliachiwa kwa kiapo maalum cha mahakama, Jumanne iliyopita ambapo watakuwa chini ya uangalizi maalum wa jeshi la polisi.

CHANZO: GAZETI LA RISASI

Comments

comments

You may also like ...