Header

Adele agawana tuzo yake ya Grammy na Beyonce

Adele akiwa ameigawanisha Tuzo yake ya Grammy.

Mwanamuziki kutoka Uingereza Adele anaonekana kukataa tuzo ya Grammy aliyotunukiwa kwa kuwa na albamu bora ya mwaka na Badala yake amesema Beyonce ndiye aliyestahiki zaidi kutunukiwa tuzo hiyo.

Adele akiwa ameigawanisha Tuzo yake ya Grammy.

Adele alishinda tuzo hiyo kwa albamu yake ya ’25’ ambayo imevuma sana Duniani, lakini ameawambia watazamaji  waliohudhuria kwamba, “Haiwezekani kwangu kupokea tuzo hii”.

“Ni heshima kubwa sana kwangu na nashukuru, lakini Beyonce ndiye mwanamuziki bora maishani mwangu”.Alisikika akisema Adele

Ushindi wa Adele dhidi ya Beyonce bila shaka utachocheza zaidi malalamiko kwamba tuzo za Grammy huwabagua wasanii weusi.

Wasanii kadha wa kadha wakiwemo Frank Ocean na Kanye West, waliamua kususia sherehe za mwaka huu za kutoa tuzo kwa washindi kwa msingi huo.

Ocean hata alikataa kuwasilisha albamu yake maarufu ya Blonde ishindanie tuzo akisema tuzo za Grammy hazionekani “kuwakilisha vyema watu wa eneo ambalo nimetoka mimi, na kudunisha watu ambao ninadunisha”.

Miaka miwili iliyopita, West aliondoka kwa hasira jukwaani baada ya Beyonce kukosa kutangazwa mshindi kwa albamu yake kwa jina Beck’s Morning Phase.

Hata hivyo, albamu ya Adele ya 25 bila shaka ndiyo iliyouza nakala nyingi zaidi miongoni mwa zilizokuwa zinashindania tuzo hiyo. Iliishinda albamu ya Lemonade yake Beyonce kwa 10 kwa 1.

Haijabainika iwapo Adele ataikataa rasmi tuzo hiyo au watagawana kama vyombo vingi vya habari vinavyoripoti na endapo atafanya hivyo basi itakuwa ni mara ya pili kwa jambo kama hilo kutokea.

Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1990, pale Sinead O’Connor alipoikataa tuzo ya albamu bora mbadala kwa albamu yake I Do Not Want What I Have Not Got, na kudai sherehe hizo zilikuwa zimeingiliwa sana na “biashara”.

Adele ameshinda jumla ya Tuzo Nne za Grammy usiku wa jana Ingia HAPA kusoma orodha yote ya washindi wa Tuzo hizo.

Comments

comments

You may also like ...