Header

Bongo Movie yafikiria namna nyingine ya kuuza filamu zao…

Sanaa ya Tanzania inawakilishwa na vitu vingi moja kati ya vitu hivyo ni pamoja na uwepo wa Filamu ambayo stori nyingi za mtaani zinadai kuwa soko la Filamu kwa sasa kama limeshuka yaani halifanyi vizuri kama miaka michache iliyopita.

Sasa mmoja kati ya ‘Queens’ kutoka Bongo Movie Irene Uwoya amesema kuwa miongoni mwa sababu za soko la filamu kuonekana kama limelala ni misiba mfululizo waliyoipata na kuwafanya wengi wao kuwa kama kupigwa na ganzi ingawa wapo wengine wamejiwekeza kwenye tamthilia zaidi.

Akijibu swali aliloulizwa na Gardner G Habash kwenye kipindi cha JAHAZI ,kuwa kama kuna mpango wowote wameupanga  kama tasnia ya filamu ili kuisogeza mbele zaidi Uwoya amesema >>’Kwa sasa tuna mpango wa kuweka movie kidigital zaidi isiwe tu mtu anaenda sehemu ananunua,mpango wetu ukikamilika itakua mtu anaweza kununua filamu hata kwa kupitia huduma za kipesa kwenye simu yake’

Kama teknolojia hii ikitimia itakua haina utofauti na ile ambayo inatumika kwa sasa na watu wengi,kwenye kununua umeme kupitia simu.

Uliiona hii ya TID kukiri wazi mbele ya Mkuu wa Mkoa na Watazamaji kuhusu kutumia Dawa za kulevya?Bonyeza play kutazama..

Comments

comments

You may also like ...