Header

Nuh Mziwanda awajibu wale wanaoingilia mapenzi yake na Mkewe…!

Staa wa Hit single ya Jike Shupa , Nuh Mziwanda leo kawatolea uvivu wale wote ambao wamekua wakisema maneno mengi juu ya uhusiano wake na Mkewe anaeitwa Nawal ya kuwa anamsaliti na huenda amerudiana na aliyekua mpenzi wake Shilole.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nuh Mziwanda ameandika >> ‘Binadamu haishiwi maneno’kuamua kuoa si jambo dogo Kama wao wanavyofikiria ‘mana wangeshaoa pia ‘ila ni hekima zako ,busara na tabia njema ulitunukiwa na Mungu baba’

‘Kuna msemo unasema Maisha popote na una maana kubwa sana kwangu ‘iwe jangwani,vitani,majinj,nitatafuta ridhiki mradi upendeze na kupata shibe wewe na mwanangu inshaalah (NATAFUTA FOR YOU NAWAL).nakupenda sana Mke wangu’ Nuh Mziwanda.

Comments

comments

You may also like ...