Header

Wema Sepetu afunguka, ‘Nashukuru kwa dua zenu, zimenisaidia’

Ikiwa ni siku takriban tatu tangu awe mtu huru baada ya kukaa selo kwa takriban wiki nzima kutokana na kuhusishwa na matumizi ya dawa za kulevya, Wema Sepetu amefunguka.

Hiki ndicho alichokiandika kwenye Instagram:

Mimi na familia yangu tunapenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zetu za dhati kwa wote mlioshirikiana nasi kwa hali na mali katika kipindi hiki kigumu tulichopitia. Najua wengi mlikua mnaniombea, nashukuru kwa sala na dua zenu kwani zimenisaidia kwa kunipa nguvu wakati nikiwa kwenye wakati mgumu sana kwenye maisha yangu. Napenda kuwashukuru mashabiki wangu wote duniani kwa kuniamini na kusimama na mimi kwa kipindi chote hiki, pia napenda kuwashukuru wasanii wenzangu wote. Asante sana kwa mwanasheria wangu Alberto Msando kwa kunisimamia na kuwa na mimi bega kwa bega wakati huu mgumu. Nakuombea kwa Mungu akupe moyo huohuo wa kuwatetea wanyonge. Asante sana.
Familia ya marehemu Mzee Issac Sepetu tunasema asanteni sana.

Kwenye kesi yake, Wema aliyetoka kwa dhamana ya shilingi milioni tano anakabiliwa na kosa la kukutwa na bangi nyumbani kwake pamoja na mengine mawili.

Comments

comments

You may also like ...