Header

TIMMY Amtumia ‘DELA’ Ujumbe Wa Valentine ila Kwa Mafumbo

Msanii mkali wa humu nchini TIMMY T DAT ambaye sasa hivi anafanya vizuri na kazi yake mpya ‘Trikideh’, Jana pia hakuwachwa nyuma kwenye shughuli nzima ya siku ya wapendenao. Mkali huyu wa kuchana kupitia mitandao yake ya kijamii aliandika “Happy valentines dear. we met for a reason and I treasure each moment we spend together. You are very much loved and appreciated. you mean a lot to me and I thank God that I met you.. “Mbona unafanyanga nasikwa na mafeeling?” #trickydeh “. Kwa mtu wa kawaida ni vigumu kuelewa ujumbe huu ila hapo pa ‘unafanyanga nasikwa na mafeeling?’ ndio basi linatupa jibu letu ni Nani haswa ujumbe huu ulikuwa unatumiwa maana nyimbo ya DELA iliyofanya vizuri na ikamtambulisha vizuri ni ‘Mafeelings’. Za chini ya carpet zinadai kuwa TIMMY & DELA ni wapenzi ila wawili hao hawajai kutoka wazi wazi na kukubali kuwa wanatoka.

Comments

comments

You may also like ...