Header

Facebook kuja na huduma mpya ya kutafuta na kuomba kazi kwa watumiaji wake

Hakuna ubishi kuwa mtandao wa Facebook ndiyo mtandao unaokua kwa kasi zaidi Duniani ukiachilia mbali Mkwanja faida unayopata kwenye matangazo lakini pia mtandao huo hata ubunifu wake ni wa hali ya juu ukilinganisha na mitandao mingine ya kijamii .

Image result for facebook on my phone

Habari nzuri kwa watumiaji wa mtandao wa facebook ni kwamba kwa sasa watakuwa na nafasi ya kuweka nafasi za kazi na kuomba maombi ya kazi husika moja kwa moja kwenye mtandao huo.

Facebook wamesema huduma hiyo itakuwa ni kwa yale makampuni yenye kurasa za kibiashara tu yaani (Business Pages) ambapo watu watakao kuwa wame’like kurasa hizo ndiyo watakaopata nafasi ya kutoa maoni (comments) na ku’Apply kazi iliyotangazwa na Kampuni husika moja kwa moja kwenye mtandao wa Facebook.

Huduma hiyo inatarajiwa kuzinduliwa leo kwa kuanza na nchi za Marekani na Canada na baadae kusambaa Duniani kote ila bado haijatangazwa ni lini huduma hiyo itaingia Afrika,kumbuka huduma hii kwa zile kurasa za kibiashara tu na kama ukurasa wako haujawa wa kibiashara tafadhali badilisha ukurasa wako ili baadae ufaidi huduma hii.

 

 

Comments

comments

You may also like ...