Header

Gigy Money atoa sababu ya kumwagana na mchumba wake Mo J

Video Queen Gigy Money na mtangazaji mwenzake wa kituo kimoja cha redio nchini Moulad Alpha ‘Moj’ hatimae mahusiano yao ya kimapenzi yamevunjika baada ya mwanadada huyo kusalenda kutokana na madai kwamba mchizi alikuwa akimshushia sana kichapo mwanadada huyo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo karibu na wawili hao, Gigy amesema kwenye mapenzi yake alijitahidi kulinda penzi lake lakini  jamaa hajatulia na kila anapomuhoji kwa nini anamsaliti anampa mkong’oto.

Habari ndo hiyo, wale wameshaachana maana mara kwa mara Gigy alikuwa anapigwa kwa kosa ambalo si lake, amevumilia sasa uzalendo umemshinda,” alisema sosi.

Kwa upande wake Gigy alipotafutwa, alisema alikuwa anampenda sana Moj kwani alimuona ni mstaarabu lakini ghafla amebadilika sana.

“Kweli kupenda utumwa, mateso niliyoyapata kwa huyu mwanaume nimesalenda, kwa nini haniheshimu na ananipiga?” alisema Gigy

CHANZO:GAZETI LA AMANI

Comments

comments

You may also like ...