Header

“Kenyans Make Foreign Songs Bigger Here Than They Are in Their Countries Of Origin” – BIEN Awapa Makavu Wakenya Wanaosupport Muziki Wa Nje Kuliko Wa Humu Nchini

Msanii Bien -Aimé Baraza kutoka kundi la Sauti Sol ameamua kuliweka wazi swala ambalo wengi huwa wanaogopa kuzungumza wazi wazi wanaishia kuropoka tu kwenye group za ‘Whatsapps’. Mkali huyo wa Sauti Sol kupitia mtandao wake wa facebook  aliandika “Kenyans are such superstars. We make foreign songs bigger here than they are in their countries of origin. . Happy dustbin for foreign bullshit day to you all. Hope you smell the trash soon”, post hii ilichukuliwa kama dogo kwa wakenya ambao wanapenda ku support muziki wa nje kuliko wa humu ndani. Kwa muda sasa wakenya wamekuwa wakikashfiwa kwa kupenda muziki wa nje kuliko wa kwao. Haya huonekani kupitia ma tamasha mbali mbali na pia wakati mwingine unapata wakenya wanaponda muziki wa wakenya wenzao.

Comments

comments

You may also like ...