Header

Baada ya Nay wa Mitego kuachia wimbo mpya,Basata wampigia simu na kumwambia maneno haya..

Muda wetu ni jina la wimbo mpya ya Nay wa mitego ambayo kaiachia rasmi Feb 16 kwenye Radio/TV na kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na baada ya kuachia moja kati ya simu alizozipata ni kutoka Basata.

Simu hiyo imepigwa na katibu mtendaji wa BASATA Mr Godfrey Mngeleza akimpongeza kwa maudhui mazuri ya wimbo huo na Nay kupitia XXL ya Clouds FM amesema>>‘Nimepokea simu nyingi lakini Miongoni mwa watu walionipigia simu baada ya kuusikia wimbo huu ni Katibu wa Basata kasema una maudhui mazuri,hii ni mara yangu ya kwanza kusifiwa na Basata’.

Ikumbukwe kuwa Nay wa mitego mara kadhaa amekua akiingia kwenye mgogoro na Baraza hilo mpaka kufikia kufungia baadhi ya nyimbo zake kama ‘Pale kati’ na zingine baadhi.

Comments

comments

You may also like ...