Header

Bongo Bhangra haijafa – Big Jahman

Katikati ya miaka ya 2000 moja kati ya miziki iliyoingia na kuwa gumzo ni pamoja na muziki ulioitwa Bongo bhangra ambao ulikua ni kama mchanganyiko wa muziki wa Bongo na India ambao ulizaa nyimbo kadhaa kama Regina na Bongo Bhangra zilizoimbwa na Marehemu Steve 2K kwa kushirikiana na baadhi ya watu akiwemo Akili the brain na Big Jahman.

Maoni mengi ya wadau wa muziki,wamesema kuwa muziki huo haupo na kama upo hausikiki kwa sababu ya kufariki miongoni mwa muasisi wa muziki huo Steve 2K,kwenye XXL ya Clouds FM mmoja kati ya wasanii waliokua wanafanya muziki huo Big Jahman amesema kuwa >>’Yale matatizo yalipotokea kati ya marehemu Steve 2k na Producer  wetu Casto studio ilibidi ifungwe na Casto ndiye alikua producer wetu kwa kipindi kile”

‘Ilibidi tutulie japo Akili alikua producer lakini haimaanishi muziki ulikufa au style ilikufa,tunaendelea kufanya Bongo bhangra,bado Bongo bhangra ipo na itarudi japo tunammis sana mshkaji wetu Steve 2k na alikua na mchango mkubwa sana kwenye muziki wa bongo bhangra’.

Kama ulikua huujui muziki wa Bongo Bhangra,hii ni moja kati ya singo zilizowahi kufanya vizuri sana,Singo inaitwa Regina.

Comments

comments

You may also like ...