Header

Hiki ndicho asichokipenda Shaa kwenye Muziki wa Bongo Fleva

Msanii wa bongo fleva Shaa ni moja ya Wasanii wa Kike ambao wanafanya vizuri sana kwenye Muziki lakini kuna kitu ambacho kwenye sanaa hapendi kabisa kukisikia kutoka aidha kwa mashabiki au kwenye Media na kitu hicho ni kufananishwa na wasanii wengine wa kike.

Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Shaa amesema mambo ya kushindanishwa na wasanii wenzake kama Vanessa na LadyJay Dee na wengine kwake hayana umuhimu kwani kufanya hivyo ni kuendeleza mashindano ya kuzidi kunyong’onyesha wasanii wa kike ambao ni wachache kwenye Tasnia.

“Sipendi kulinganishwa na wasanii wenzangu wa kike kama Vanessa na Lady Jay Dee kwani kufanya hivyo kutazidi kuwapoteza wasanii wa kike ambao ni Wachache kwenye Tasnia na hii haijalishi iwe ni Media au kwa Mashabiki”Alisema Shaa Kwenye kipindi cha eNEWS cha EATV.

Comments

comments

You may also like ...