Header

The Amazing kuongeza idadi ya members? Sikia alichojibu Izzo Bizness

Miongoni mwa makundi yanayotawala anga la Bongo kwa sasa, ni Kundi la The Amazing linaloundwa na Wakali Izzo B pamoja Na Abela Music. Kundi hilo limejizolea umaarufu mkubwa kwa kipindi kifupi kutokana na kazi zao,umaarufu ambao umefanya wafuatiliwe zaidi na mashabiki ambao wanatamani kufahamu vitu vingi kutoka kwao.

Miongoni mwa vitu ambavyo mashabiki wanatamani kufahamu kutoka kwa The Amazing,ni je kundi hilo litaongeza idadi ya Members kwenye kundi hilo? Swali ambalo limejibiwa na Izzo B.

“Kwa saa hizi bado ni mapema,kwasababu kundi lenyewe tunapambana kulisimamisha kwa level za juu zaidi..kuna miziki mingi tunarekodi,so tunasubiri kuwaaminisha watu kwa kile ambacho tunafanya,” Izzo ameiambia Dizzim Online.

Mpaka sasa kundi hilo limeshafanya kazi na producers Abbah na Dupp japo Izzo amedai kuwa wao wapo tayari kufanya kazi na producer yoyote japo ngoma yao ijayo imefanywa pia na Abbah.
Attachments area

Comments

comments

You may also like ...