Header

Huyu ndiye Mungu ambaye Nay wa Mitego anamuabudu

Mkali wa mitaa ya Manzese, Nay wa Mitego ameachia ngoma mpya ‘Muda Wetu’ ambayo ina baadhi ya mistari iliyozua utata tayari.

Miongoni mwa mistari hiyo,ni ule ambao Nay anasema, “Hivi mnamuabudu mungu gani asiyewajibu kila siku,Bora muwe wapagani ka vipi muabudu kuku/Mungu wangu yuko fasta,nikitaka nyumba ananipa gari ananipa,siamini mapasta,” amechana Nay.

Dizzim Online imepiga story na Nay kupata ufafanuzi wa huo mstari ambao umekuwa na maswali mengi sana.

“Mungu wangu nadhani ananiskiliza. Mungu wangu nikimuomba ananipa kile ambacho namuomba.Ni vile tu nikimfikishia maombi yangu na kuongeza spidi kwenye kazi. Huwa ananipa kile nnachokitaka, sasa sijui hao wengine wanamuomba mungu gani ambaye hawasikilizi,hawatimizii kile ambacho wanamuomba,” amesema Nay.

Pia Nay amegusia suala la wasanii kubebwa, unaweza kumsikiliza zaidi hapo juu.

Comments

comments

You may also like ...