Header

Instagram kuongeza idadi ya Picha za Kuposti kwa wakati mmoja

Kila kukicha mtandao wa Instagram unazidi kuboresha huduma zake ili kuendana na matakwa ya watumiaji kwani tumeona mabadiliko ya #InstaLive na sasa wapo karibu kuleta mabadiliko mengine ya kuposti picha nyingi kwa muda mmoja tofauti na mfumo wa sasa hivi wa kuposti picha m0ja moja.

Kwa watumiaji wa Facebook na WhatsApp ni rahisi sana kuposti picha nyingi kwa wakati mmoja lakini kama unatumia mtandao wa Instagram itakulazimu kuposti picha moja moja hata kama una picha nyingi za kuposti kwa muda huo.

Ila kwa ujio huo Instagram itakuwa imerahisisha kwa watu ambao hupenda kuweka picha za matukio kama harusi au Tamasha kwani watakuwa na uwezo wa kuweka picha nyingi kwa wakati mmoja.

Hata hivyo Instagram hawajataja tarehe rasmi ya kuzindua huduma hiyo ingawaje wamesema ni mwaka huu kwahiyo endelea kutufuatilia kwani tutakujuza hapa hapa tukishapata taarifa zaidi juu ya ujio huo.

CHANZO: Mtandao wa The Next Web

Comments

comments

You may also like ...