Header

Ni upumbavu kuwapa interview hawa wanaojiita fulani fulani Rapper,Mi sipendi – Madee.

Kwenye historia ambazo mwaka 2017 zimebaki ni kuanzishwa kwa vizazi vipya vya watu wanaofanana na mastaa na kujiita marapa kwa mfano Kibongobongo tumeona Harmorapa na yule ambaye anajiita Chiburapa ambaye bado hajafanikiwa kutoa wimbo wowote.

Sasa mmoja kati ya wakongwe kwenye Bongo fleva Madee amesema yeye hapendezwi na jamaa hao ambao wameibuka sasa na kutumia majina ya watu maarufu na kumalizia na neno rapa>>’Huo ndio ujinga ambao mimi naupinga kila siku,watu wa habari kupoteza muda kwa watu ambao tunaona wanalazimisha vitu ambavyo sivyo’

‘Huwezi kuja tu siku mtu ajiite Askofu rapa ni upumbavu kupoteza muda kumpa interview mtu kama huyo kumuacha aandikwe,huo muda tungetafuta watu wenye vipaji vya ukweli mtaani tungewapa promo kama hiyo naamini tungekua na wanamuziki wengi wazuri lakini vitu vya kijinga vinapewa sana nguvu lakini vitu vya maana vinabaniwa mi sipendi hii’

 

Comments

comments

You may also like ...