Header

TFF yatoa onyo kali kwa Timu za Daraja la Kwanza

Shirikisho la mpira nchini TFF limetoa onyo kali kwa Timu zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kuwa halitavumilia kwa timu ambazo zitasusia kwenda uwanjani kucheza Mechi zao kama ratiba ilivyopangwa.

Onyo hilo limekuja baada ya Baada ya Timu shiriki kutoa madai kuwa ratiba ya michezo hiyo imepangwa kwa upendeleo ili baadhi ya Timu kupata matokeo hivyo kuna Tetesi kuwa timu hizo zimegoma kucheza michezo iliyosalia.

Kuna taarifa kuwa baadhi ya timu za Ligi Daraja la Kwanza zimepanga kutokwenda kucheza na wapinzani wao kwa sababu mbalimbali wanazozijua wao wenyewe. TFF haijaona sababu za msingi hadi sasa, hivyo inaonya mipango ya timu hizo kwani inaona hakuna tafsiri nyingine zaidi ya dhana ya kupanga matokeo. Ikithibitika kinagaubaga, timu husika au viongozi wakataopanga matokeo adhabu yake ni kufungiwa maisha kwa mujibu wa kanuni.“Onyo la TFF

Comments

comments

You may also like ...