Header

Chelsea uso kwa uso na Man United robo fainali ya Kombe la FA

Ratiba ya michezo ya robo fainali ya Kombe la FA imetoka ambapo Chelsea itacheza na Manchester united, Middlesbrough itakutana na kati ya Huddersfield na Manchester City, tottenham itakutana na Millwall na Suton uso kwa uso na Arsenal au Lincoln.

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema Chelsea inapeleka nguvu zake kwenye Kombe la FA kwa kuwa ”tayari ni mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza”.

Mourinho ameendelea kujijitea kwa kusema ” itanibidi kucheza na Saint Etienne na kucheza fainali Kombe la EFL na nina matumaini ya kucheza na mpinzani mwingine kwenye ligi ya Europa ninahitaji kupambana kupata nafasi kati ya nne za kwanza kwenye ligi kuu.”

Mara ya Mwisho Chelsea Kukutana na Manchester United Kwenye Kombe La FA Ilikuwa ni Aprili 1 Kwenye Dimba la Stamford Bridge Mwaka 2013 na mchezo huo uliisha kwa Chelsea kuibuka na ushindi wa Goli 1-0,Goli pekee lililofungwa na Demba Ba.Je,Manchester United watalipiza Kisasi hapo March 11 pale darajani?

Michezo hii itachezwa kati ya tarehe 11 na 12 ya Mwezi March.

Comments

comments

You may also like ...