Header

Madee aeleza sababu ya kulia katikati ya Tamasha la burudani…

Rais wa Manzese ‘Madee’ ni miongoni mwa watu waliomake headlines wikiendi iliyopita baada ya kutoa machozi katikati ya perfomance ya muimbaji wa zamani wa taarabu Bi.Mwanahela wakati akiendelea kwenye usiku wa Love,Melodies &Light,Watu wengi hawakujua sababu ya Madee kulia mbele ya watu wengi kiasi kile.

XXL ya Clouds FM imempata Madee mwenyewe na kuelezea kilichosababisha yeye kutoa machozi ukumbini hapo wakati wa perfomance ya Bi.Mwanahela amesema >>’Ule wimbo ambao alianza kuimba ndio ulikua ndio wimbo pendwa kabisa nyumbani kwetu wakati mimi nakua’

‘Nimeumia sana baada ya kuona anapandishwa jukwaani kuimba, kwa mfano angekua mzima angekua kashaimba na kushuka mwenyewe, nimeambiwa kuna show zingine anashindwa kufanya kwa sababu zinakua hazina maandalizi mazuri kama hii,Naomba kama kuna kitu kinaweza kufanyika basi kifanyike ili mama apate nafasi ya kutembea kama zamani’

‘Akiwa anaimba vile mimi inaniumiza sana kwa sababu nawaza angekua mzima angekua anajishughulisha na muziki na mpaka sasa tungekua tunaona nyimbo zake mpya,siwezi kujielezea yule mama Mungu anisaidie tu siku moja niweze kumsaidia’. -Madee.

Bi.Mwanahela ni miongoni mwa waimbaji wakongwe wa muziki wa taarabu,waliowahi kuimba na kutunga nyimbo kadhaa ikiwemo Mahaba ya dhati na Nimezama nyimbo ambazo alikua kuzirudia Ray C baadae.

Bi.Mwanahela

Kwa mapenzi ya mwenyezi Mungu Bi.Mwanahela kapoteza uwezo wa kutembea kwa sasa lakini uwezo wa sauti yake haujachuja mpaka sasa,unaweza kubonyeza play kusikiliza miongoni mwa nyimbo zake alizowahi kutoa.

Cheki Zari alivyokuwa anafanya shopping ndani ya Gsm Mall Pugu Road Dar es salaam.

Comments

comments

You may also like ...