Header

‘Tasnia ya Wizara ninazoziongoza inakua’ – Waziri Nape Nnauye.

Waziri wa habari,sanaa,utamaduni na michezo, Nape Nnauye ni miongoni mwa wageni wa heshima waliopata nafasi ya kukaa meza kuu kwenye tamasha la Love,melodies&lights ambapo kabla ya kuelekea sehemu ya kuketi alipata nafasi ya kupitia kwenye red carpet ya event hiyo.

Kwenye Redcarpet maswali aliyokutana nayo ni pamoja na neno lake kwenye upande wa sanaa na burudani anaionaje kwa sasa ambapo alijibu>>Jambo moja linalonipa faraja kwamba tasnia inakua ukiona kuna matukio ya burudani mbalimbali na Watanzania wanaitikia ujue tasnia inakua,so na mimi nimekuja kushuhudia ukuaji huu wa tasnia’

‘Watanzania tumejaaliwa sana kuwa na vipaji vizuri,kwangu mimi kwenye nyimbo za Ben Pol naupenda Moyo mashine‘ kwenye upande wa nyimbo za Barakah Waziri Nape anaupenda wimbo wa Siachani nawe huku akiusifia na wimbo wa Ditto wa moyo sukuma damu.

Comments

comments

You may also like ...