Header

Shamsa Ford amkumbuka Mmewe ‘Chidi Mapenzi’ kwa ujumbe huu mzito

Muigizaji wa Bongo Movie Shamsa Ford amemkumbuka mmewe Chidi Mapenzi kwa kumtumia ujumbe mzuri ambao ulikuwa na tafsiri ya kwamba ingawaje amepatwa na matatizo lakini bado yupo nae kwenye kila hali.

   Shamsa Ford na Chidi Mapenzi

Shamsa kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuna watu wanamdharau kwa sababu ya tatizo lililompata Mme wake lakini yeye anaamini haya ni matatizo ambayo yanakuja na kupotea.

“Nilipoolewa nilijua ipo siku nitapitia hivi vitu huzuni,furaha, maudhi, kudharauliwa, kuchekwa na nk.ila pamoja na yote hayo haitabadilisha mapenzi yangu kwa mume wangu kipenzi. Nina amini kuwa wewe ni mume aliyenipa Mungu na wala Mungu hakutukutanisha kwa bahati mbaya.”Ameandika Shamsa Ford.

Aliendelea kusisitiza kuwa Chidi ndiye chaguo lake sahihi kwa kuandika “Dunia nzima ikuzomee na kuamini kile wanachoamini lakini jua una mke anayekupenda kwa dhati .Ninakujua, ninakuamini na kukupenda sana ndomaana niliolewa na wewe kwasababu nilijua utakuwa baba bora kwa mwanangu kama ambavyo ulivyo sasa..Nina amini Mungu anapotaka kukupeleka sehemu anayoitaka yeye lazima akupitishe kwenye mitihani. Hii ni mitihani ya Mwenyezi Mungu na nina imani inshaallah yatapita..Nakupenda sana mume Wangu kipenzi Rashidi..

Mmewe na Shamsa Ford Chidi Mapenzi leo anafikishwa mahakani kujibu shutuma za kujihusisha na Biashara ya Madawa ya Kulevya baada ya kushikiliwa na polisi tangia wiki iliyopita.

Comments

comments

You may also like ...