Header

‘Sijawahi kumkubali Fid Q kwenye Freestyle’-Young Killer

Rapa kutoka Mwanza Young Killer amefunguka na kusema hajawahi kumkubali rapa Fareed Kubanda  Fid Q kwenye kufanya mitindo huru kwa kuwa hajawahi kumuona mkali huyo wa hip hop Bongo akifanya mitindo huru.

Image result for Fid q na Young killer

                                             Fid Q na Young Killer

Young Killer amesema anawakubali sana Nikki Mbishi, Godzilah pamoja na marehemu Albert Mangwea kwa kufanya ‘Free style’ sababu anatambua uwezo wao katika nyanja hiyo.

“Sijawahi kumkubali Fid Q kwa ‘free style’ sababu sijawahi kumuona akifanya hivyo ila niliowahi kuwaona wakifanya mitindo huru nampenda sana Nikki Mbishi, GodZillah pamoja marehemu Albert Magwea” alisema Young Killer kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio.

Young Killer na Fid Q walishawahi kufanya Kolabo ya wimbo wa Agosti 13 na amesema kwa sasa anatamani sana kufanya ngoma na Mbunge wa jimbo la Mikumi Professor Jay.

Comments

comments

You may also like ...