Header

Gosby ataja list ya marapper anaowakubali Bongo

Tanzania na Afrika kumekuwa na uchache wa wasanii wanaoweza kutaja na kusifia kazi za wasanii wenzao. Wengi wamekuwa wakishindwa kutaja kwa majina wasanii wanaowakubali tofauti na wasanii wa nje ya Afrika ambako wengi wamekuwa wakiweka wazi wasanii wenzao wanaohisi wanafanya vizuri.

Akiongea na Dizzim Online, Gosby amewataja ma rapper wenzake wanao fanya vizuri. Akijibu swali letu Gosby amesema, “Fid Q amekuwa akiachia ngoma kali, Joh Makini ametoa ngoma kali pia Mwana FA ametoa ngoma kali pia.”

Kwenye mahojiano naye, Gosby amezungumzia sababu za mixtape yake Swaghili kutotoka hadi sasa. Msikilize zaidi hapo juu.

Comments

comments

You may also like ...