Header

Nikki wa Pili atoa funzo kwa BASATA ‘Kiwanda cha Sanaa ya Soko hakipendi Maadili’

Rapa kutoka Arusha Nikki wa Pili haishiwi kutoa maoni ya kujenga hususani linapofikia suala la kuzungumzia Sanaa kwani huwa jambo hilo linamgusa moja kwa moja kama msanii.

Wiki iliyopita Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) liliandika Makala iliyochapishwa na Gazeti la Mwananchi iliyokuwa na lengo la kuelimisha maadili kwenye Sanaa kuwa yalindwe na Jamii anayotoka msanii husika ili kulinda mmonyoko wa Maadili kuanzia kwenye Sanaa na hata jamii kiujumla.

Sasa baada ya Makala hayo Nikki wa Pili ametoa ushauri na maoni yake ambayo aliangalia vitu vikubwa vinavyoweza kuongeza tatizo la mmonyoko wa Maadili kwenye Sanaa yetu kuendelea kuota mizizi.

Kwanza alianza kusema Wanasiasa wamechangia kwa kiasi kikubwa kuendeleza mmonyoko wa Maadili kwenye  Sanaa kwani wanawatumia  wasanii kwenye kipindi cha Kampeni na kuimba hata nyimbo Maadili unadhani tatizo litaishaje “Viongozi vyama vyote hupata kura kwa kampeni za wasanii bila kujali maadili yao.mpaka kwa nyimbo za matusi.basata bado mnahoji madili he he“ameandika Nikki wa Pili kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Aliendelea kuzungumzia Suala la Madawa ya kulevya kama ni moja ya vitu vilivyosambaratisha maadili kwenye Sanaa na kusema Sanaa yetu hapa Tanzania ukizungumzia vitu vya Maadili ni ngumu sana kuuza kazi zako kuliko vile vitu vinavyobomoa Maadili .

Kuongea madawa na sanaa ni Kuongea juu ya maadili..kiwanda cha Sanaa ya Soko hakipendi Maadili…maadili yanasemakana haya uzi“Ameandika Nikki wa Pili kwenye ukurasa wake wa Twitter.

 

Comments

comments

You may also like ...