Header

Diamond Platnumz aitwa TRA kuhojiwa..

Taarifa iliyoanza kutoka Feb 22 na kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja na hii ya Diamond Platnumz kuitwa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya mahojiano mafupi.

Kupitia post yake aliyoipost instagram Diamond Platnumz ameandika >>’Mapema leo nilipo ripoti makao makuu ya TRA baada ya kuitwa ili kuelezea ni namna gani nayapata mapato yangu na namna gani nalipa kodi ya serikali’.

Hii itakua ni mara ya pili kwa Diamond Platnumz kuitwa na mamlaka hiyo,mara ya kwanza ilikua mwaka mmoja uliopita ambapo Mamlaka hiyo ya Mapato ilimkadiria kodi ambayo Diamond alitakiwa kulipa na kwa bahati nzuri Diamond Platnumz aliilipa hiyo pesa.

Comments

comments

You may also like ...