Header

G-Nako atoa ushauri kwa waongozaji wa video za muziki Bongo

Wakati ambao wasanii wa kibongo wamekuwa wakipata lawama kuhusu kwenda kufanya video zao nje, kumeibuka lawama mpya juu ya video directors wa kibongo. Hii ni baada ya wao kuonekana wakitumia maeneo yale yale katika video tofauti tofauti.

Na pia kumekuwa na uchache wa mavideo queen, hii imeonekana baada ya video queen hao kutumika kwenye video nyingi.

Baada ya kuliona hilo G-Nako ameamua kutoa ushauri kwa video directors wa kibongo.

“Hili suala watu wanatakiwa kulichukulia kama kazi na pia suala la locations kutumika zile zile mi nahisi ni wakati sahihi watu kupanua mawazo zaidi,” ameiambia Dizzim Online.“Na pia hili suala sio la directors pekee sio mbaya msanii akimshirikisha mawazo yake director wake,” amesisitiza.

Pia G amezungumzia ujio wa ngoma yake mpya atakayoitoa hivi karibuni ambayo amemshirikisha Jux.
Kwenye mahojiano haya pia rapper huyo amezungumzia uhusiano wake na member mwenzake wa Weusi, Lord Eyez.

Comments

comments

You may also like ...