Header

Producer Mr T Touch amtaja ‘Role Model’ wake

Hakuna ubishi ukitaja watayarishaji wa muziki 10 bora kwa mwaka jana huwezi kumuacha  Mr T Touch na hii ni kutokana na ngoma kali alizotengeneza.

Akizungumza na DizzimOnline Boss huyo wa Sound Touchez amesema huwa anavutiwa na maproducer wengi sana ndani na nje ya nchi lakini kwake mtu ambae amemshawishi zaidi ni Dr Dre.

Huwa najifunza vitu vingi kutoka kwa maproducer mbalimbali lakini producer ambae ananivutia sana na amenishawishi sehemu kubwa ya maisha yangu ni Dr Dre namkubali sana“Amesema Mr T Touch.

Mr T Touch kwa Mwaka huu tayari ametengeneza Hits kibao ikiwemo wimbo wa Mazoea wa Billnass na Mwana FA.

 

Comments

comments

You may also like ...