Header

Kuelekea pambano la Simba na Yanga,Kocha wa Simba OMOG apunguza ukali wa Mazoezi

Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog amekwenda kushusha ukali wa mazoezi ya kikosi chake kilicho kambini mjini Zanzibar kujiandaa na mechi ya Jumamosi dhidi ya watani wao Yanga.
Omog ameanza kupunguza ukali wa mazoezi na ndani ya siku hizi tatu, inaonekana watakuwa na mazoezi mara moja kwa siku badala ya mara mbili.
Kweli kwa siku mazoezi yalikuwa ni siku mbili mfululizo, lakini sasa mazoezi yamekuwa mara moja kwa siku,” alisema mmoja wa wachezaji wa Simba.
Pambano la watani wa jadi litafanyika Jumamosi hii tarehe 25 Februari,Katika mechi ya kwanza Simba na Yanga zilitoka kwa sare ya 1-1, Simba wakishawazisha dakika za mwishoni kwa bao la Shiza Kichuya ambaye alipiga mpira wa kona, ukajaa moja kwa moja wavuni.

Comments

comments

You may also like ...