Header

Madee aipa tano ngoma mpya ya Nay wa Mitego ‘Muda Wetu’

Ni ngumu sana kumuona Madee akitangaza hadharani kukubali wimbo wa hasimu wake Nay wa Mitego hii ni kutokana na wawili hao kupishana kauli mara kwa mara lakini kwa wimbo mpya wa Mr NAY ‘Muda Wetu’ Madee amekubali kuwa wimbo huo ni mzuri na ameukubali.

Madee alisema ni wimbo mzuri kwa yeye anavyouona ingawaje akatoa angalizo kuwa mashabiki nao wana nafasi ya kujaji wimbo huo kwani haijalishi mtu mmoja akitoa maoni ya ndiyo watu wote watakuwa na mtazamo huo.

Aaaahhh bonge la nyimbo yaani kali,ni bonge la ngoma“alijibu baada ya kuusikiliza wimbo huo na aliulizwa kama wimbo huo unaweza kupenya Madee alisema “Hilo ni suala lenu nyie watu wa media kama mtatumia nguvu nyingi mnaweza mkawashawishi watu wakaupenda ila kama mtapiga wimbo huo kama wasanii wengine tutaona

Mwanzoni mwa mwezi huu Nay wa Mitego kupitia Kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio alitoa Maoni juu ya wimbo mpya wa Madee ‘HELA’ kuwa ni wimbo mbaya kitendo ambacho kilimsukuma Madee nae aombe mahojiano mapema baada ya Nay wa Mitego kutoa wimbo wake.

Madee aliendelea kusisitiza kwenye mahojiano yake na Planet Bongo kuwa yeye ndiye rais wa Manzese na hatatokea Rais mwingine kwani yeye ni kama Mugabe.

 

Comments

comments

You may also like ...