Header

Manchester United yatinga hatua ya 16 Bora ya Europa League

Klabu ya Manchester United imetinga hatua ya 16 bora kwenye michuano ya Europa League, kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Saint-Etienne ya Ufaransa jana Usiku.

Man United walikuwa mbele ya mabao 3-0 kutokana na ushindi wa mechi ya mkondo wa kwanza, mabao yote yakitoka kwa Zlatan Ibrahimovic.

Kwenye mechi ya Jumatano iliyochezewa Ufaransa, Mkhitaryan alifunga dakika ya 16 kutoka kwa pasi ya mwisho ya Juan Mata,Muda mfupi baadae kabla ya kuumia misuli ya paja na kulazimika kuondoka uwanjani.

Man United imefuzu kwa jumla ya magoli 4-0 na kufanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo ya Europa League.

 

Comments

comments

You may also like ...