Header

Mchezaji huyu wa Arsenal kukaa nje ya Uwanja msimu mzima

Kiungo wa kati wa Arsenal Santi Cazorla atakaa nje ya uwanja kwa kipindi chote kilichosalia cha msimu huu kutokana na jeraha la kifungo cha mguu.

Cazorla alicheza hadi alipochechemea na kuondoka uwanjani kwenye mechi ya hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Ludogorets kunako Dimba la Emirates mwezi Oktoba mwaka.

Cazorla alifanyiwa upasuaji mwezi Desemba mwaka jana na meneja wa The Gunners Arsene Wenger alitarajia mchezaji huyo wa miaka 32 angerejea kabla ya msimu kumalizika.

Lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania atakosa mechi zote zilizosalia kwa msimu huu huku akijiandaa kwa msimu ujao kuitumikia klabu yake ya Arsenal.

Comments

comments

You may also like ...