Header

Klabu ya KRC Genk ya Mbwana Samatta yafuzu hatua ya 16 bora ya EUFA Europa League

Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji imefuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya UEFA Europa League na kumfanya Nahodha wa Timu ya Taifa Taifa Stars Mbwana Samatta kuandika historia ya kuingia kwenye hatua hiyo kubwa kabisa kuwahi kutokea kwake.

Genk wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Luminus Arena, wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Astra Giurgiu ya Romania na kuiondosha kwenye mashindano hayo kwa jumla ya magoli 3-2 baada ya michezo miwili.

Mchezo wa awali uliopigwa juma lililopita (February 16, 2017) , Genk ililazimisha sare ya kufunga 2-2 ugenini na kujiweka kwenye nafasi nzuri kwa faida ya magoli ya ugenini.

Goli pekee kwenye mchezo wa marudiano limefungwa na Alejandro Pozuelo dakika ya 67 kipindi cha pili kwa free-kick iliyozama moja kwa moja wavuni.

Kwenye mchezo huo, nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta amecheza kwa dakika zote 90 ambapo licha ya kutofunga katika mechi zote mbili za hatua ya 32 bora, Samatta amekuwa na mchango mkubwa kwa timu yake kupata matokeo.

Comments

comments

You may also like ...