Header

RIPOTI: Mtoto wa Muhammad Ali alikumbwa na Sera za Kibaguzi za Trump nchini Marekani

Vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti kwamba mwana wa aliyekuwa gwiji wa ndondi Duniani Muhammad Ali alizuiliwa na kuhojiwa kwa saa mbili katika uwanja wa ndege wa Florida baada ya kuwasili kutoka Jamaica mapema mwezi huu.

Wakili wa familia ya Muhammd Ali Chris Mancini alinukuliwa akisema kuwa kuzuiliwa kwa Muhammad Ali Jr kulihusishwa moja kwa moja na jaribio la rais Trump kuwapiga marufuku Waislamu kutoka mataifa saba ya Waislamu kuingia Marekani.

Sera ya Trump ya kuzuia raia kutoka mataifa saba ya kiislamu kutokuingia Marekani kwa sababu za Kiusalama imeathiri mamilioni ya Watu Duniani ambao walizuiliwa mapema mwezi Januari kabla ya Mahakama nchini humo kutengua marufuku hiyo.

 

Comments

comments

You may also like ...