Header

Diamond Platnumz aweka wazi sababu zilizomfanya achelewe kujiunga na Mtandao wa VEVO

Tangia aanze muziki na mpaka kujulikana Diamond Platnumz hajawahi kujiunga na Mtandao maarufu Duniani wa VEVO badala yake alikuwa anatumia Channel yake ya kawaida ya Youtube mpaka mwaka huu tulivyoona ameingia Rasmi kwenye Mtandao huo, unaweza ukajiuliza kwanini msanii mkubwa kama yeye amechelewa kujiunga kwenye mtandao huo mkubwa?.

Image result for diamond platnumz

                                              Diamond Platnumz

Diamond Platnumz amesema sababu za yeye kuchelewa kujiunga na Mtandao huo wa VEVO unaotumiwa karibia na Mastaa wakubwa wote Duniani ni kuwa kuna Madalali wengi ambao wanasababisha mapato ya Msanii kupotea na kuishia kulipwa pesa ndogo kuliko hata msanii anayetumia Youtube channel ya Kawaida.

Kuna siku niliulizwa kwanini we haupo Vevo… Nikawambia: “uwepo wa msanii @VEVO anatakiwa msanii alipwe zaidi ya alivyokuwa analipwa kwenye Youtube channel ya kawaida.. Vevo wenyewe pia wamtambue kuwa kuna msanii anaitwa Nasibu Abdul aka Diamond toka Tandale, na pia anacholipwa msanii wa Marekani kwa view moja ama tangazo lolote liekwalo mwanzo ama lipitalo katikati pindi ya utazamaji wa video hyo basi nae anapaswa kulipwa hivyohivyo…“Ameandika Diamond Platnumz kwenye Ukurasa wake wa Instagram na kuendelea kusema

Na mbali tu ya kumlipa VEVO yapaswa kwa namna moja au nyingine kusaidia kupromote maana ni biashara yao wote na kila msanii ana shabiki zake na ukubwa na nafasi yake atokapo”…..hivyo nikawambia: “siku mkiniona nipo vevo basi jua nimeyakamilisha haya, vinginevyo wacha niendee kuokota senti mbili tatu, kwenye chanel yangu ya Youtube kawaida…“Ameandika Diamond Platnumz.

Diamond amesema alikuwa kimya muda mrefu bila kuzungumzia jambo hili kwa wasanii wenzake ila leo ameona ni vyema akawajuza  kwani kuna wasanii ambao wanahitaji kujiunga na mtandao huo wa VEVO hivyo ni vyema wakafahamu machache na alimalizia kwa kuwapa ushauri.

SABABU YA KUYASEMA HAYA:Ni kutaka kuwafahamisha ama kuwaamsha baadhi ya wasanii wenzangu watambue kuwa
Mziki wetu hata kama hauko mkubwa saaaana ulimwenguni, ila Mwenyez Mungu kausaidia kuufikisha sehem flani, hivo wasanii lazma tujitambue na Tuwe na Misimamo na kazi zetu, vilevike umakini kwenye maamuzi ama hatua yoyote tutayoichkua juu ya sanaa zetu kwa sasa, maana tuliamualo leo linaweza kutujenga ama kutubomoa baadae… nafaham wasanii wengi hawakuwa wakilifaham hilo na badala yake kuingia @VEVO kupitia watu kati ama madalali na kuambulia status mtaani kuwa wako @VEVO ilhali nyuma kuna watu wanawadhurumu mamilioni ya pesa zitokanazo na jasho lao…” kwa uchungu wa kufaham namna gani inauma msanii ukinyonywa kazi yake ndio umenifanya nilizungumze hili leo, ila ukiona kwa namna moja au nyingine nimekosea Tafadhali mnisameh..“Ameandika Diamond Platnumz.

Wasanii wa Bongo wenye Akaunti za VEVO ni Vanessa Mdee,Jux,Diamond Platnumz Mwenyewe,Ali Kiba,Navy Kenzo na Gosby.

Comments

comments

You may also like ...