Header

Master Jay asema harudi tena kwenye game la Bongo fleva,sababu kamili iko hapa.

Master Jay ni miongoni mwa majina makubwa Bongo yenye heshima mpaka sasa kutokana na Wasanii wengi kupata majina kupitia studio yake ya MJ Records ambayo mpaka sasa ina zaidi ya miaka 17 na kutoa hits nyingi toka kuanzishwa kwake.

Hii inaweza isiwe taarifa njema kwa Wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya ambao inawezekana ndoto yao siku moja ni kufanya wimbo na mkongwe huyo,kupitia XXL ya Clouds FM Master Jay amekiri wazi kuwa harudi tena kwenye game>>’Kurudi mie sirudi bana nilishamaliza bana’

‘Tulishafanya ya kwetu,vijana sasa hivi wanafanya ya kwao na wanafanya vizuri sio tu Tanzania wala East Africa baki ni Afrika na International naomba niwape heshima yao,hakuna haja ya sisi wakongwe kurudi,turudi kwani vijana wamefeli,vijana bado naongea nao kwani wananiombaga ushauri’ – Master Jay.

Steve Nyerere aita Waandishi wa habari akiri ile sauti aliyokua akizungumza na Mama Wema Sepetu ni yake,ataja sababu ya kuongea vile,bonyeza play kutazama.

Comments

comments

You may also like ...