Header

Baada ya Kichapo: Charles Boniface Mkwasa awaomba radhi mashabiki wa Yanga

Baada ya Klabu ya Yanga kupoteza mchezo wao dhidi ya wekundu wa Msimbazi wikiendi iliyopita leo katibu mkuu wa klabu hiyo amewaomba radhi mashabiki na Wadau mbalimbali wa Klabu hiyo kwa kupoteza mchezo huo.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Klabu hiyo Mkwasa amewaomba Radhi kwa kutoa Press Release iliyosomeka

Young Africans Sports Club kupitia katibu mkuu wake Boniface Charles Mkwasa, inawaomba radhi wanachama wote,wapenzi na mashabiki wa klabu yetu pendwa Young Africans kwa matokeo ya jumamosi dhidi ya Simba SC kwa kupoteza 2-1.
Klabu inawaomba kuwa watulivu na pia inashukuru sana kwa utulivu mliouonesha na kutii sheria zote kwenye mchezo wa jumamosi. Matokeo haya tuliopata ni ya kimchezo kikubwa ni kupambana na michezo iliyobaki mbele yetu na kuendelea kuwapa sapoti vijana wetu kwani bado tuna mashindano mengi na michezo mingi mbeleni.
Tunaamini Mwalimu ameona mapungufu kwenye mchezo uliopita na atayafanyia kazi kuelekea michezo ijayo na tutafanya vizuri na kurejesha furaha yetu.
Uongozi unaamini wanachama na wapenzi wa Yanga wataendeleza utulivu na kuendelea kuipa sapoti timu yao kama ilivyo jadi yao.
DAIMA MBELE NYUMA MWIKO.

Imetolewa na idara ya habari na mawasiliano.
Young africa sports club.
27-02-2017

Yanga ilipoteza mchezo huo kwa kukubali kipigo cha magoli mawili dhidi ya Simba Jumamosi iliyopita kwenye mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara.

 

Comments

comments

You may also like ...