Header

Haji Manara – ‘Hatutafungwa tena na Yanga’

Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amefunguka na kusema klabu ya Yanga haiwezi kuifunga Simba sehemu yoyote ile kama mchezo utakuwa wa haki.

Haji Manara amesema hayo baada ya timu yake ya Simba kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya watani wao wa jadi Yanga katika mchezo uliochezwa siku ya Jumamosi ya tarehe 25, Februari katika Uwanja wa taifa Dar es Salaam.

Mbali na hilo Haji Manara anasema msimu huu ni lazima wachukue kombe kwani anasema hakuna timu ambayo itaiweza Simba sasa na kudai kuwa kila timu watakayokutana nayo sasa hivi ni kichapo.

“This is Simba, mliona tulicheza wangapi uwanjani, kwa dakika ngapi, wamepata goli la namna gani, tumepata magoli ya namna gani? This is Simba huwa tunataka fair game, hawa Yanga hawajawahi kutufunga kukiwa na fair game popote pale, narudia hawajawahi na hawatakuja kutufunga popote pale, hii ndiyo Simba. Na tutamfunga yoyote anayekuja hivi sasa tunahitaji ubingwa tu, na ubingwa ni lazima unafikiri nani atatuzuia? Simba tunazuilika na nani saizi” alisisitiza Haji Manara .

Timu ya Simba kwa sasa ipo kileleni mwa ligi ikiwa na pointi 54 wakifuatiwa na Yanga wakiwa na pointi 49.

Comments

comments

You may also like ...